Kiini cha mtoto mchanga  iliyogandishwa yapata miaka 24 chazaliwa salama katika mji wa Tennessee, Marekani.

Wachangiaji wasiojulikana waliacha kiini cha mtoto katika Kituo cha kuhifadhia viini cha Tennessee kiitwacho “National Donation Center”, Marekani tangu tarehe 24 Novemba 1992.

Tina Gibson aliyeolewa miaka saba iliyopita hakutaka penzi la ndoa yake iingiwe na giza aliamua kuasili kiini hicho na baada ya mwaka akajifungua salama mtoto wa kike.

“Do you realize I’m only 25? This and I could have been best friends,” Tina Gibson said.

“Je unafahamu kuwa nina miaka 25 tu, hiki kiini cha mimba na mimi tungekuwa marafiki wazuri” Alisema Tina Gibson

Tina aliiambia kituo cha runinga cha CNN kuwa bila kujali kama ni rekodi ya dunia

“I just wanted a baby. I don’t care if it’s a world record or not.”

“Nilichotaka ni mtoto tu, sijali kama ni rekodi ya dunia”

Emma Wren Gibson alizaliwa Novemba 25.

Kiini cha mtoto kilichokuwa kinashikiliia rekodi ya dunia ni ile ya miaka 20

Utaratibu wa kuchangia viini vya watoto kutoka kwa watu wasiojulikana na viini hivyo kuhifadhiwa kwa kugandishwa ili viasiliwe na mzazi/mlezi mtarajiwa asiyetaka kuzaa kwa njia za asili au asiyekuwa na uwezo wa kuzaa kwa njia za asili imeenea sana katika nchi zilizoendelea kwa sayansi hii hasa Marekani.

Utaratibu hu umekuwepo tangu mwaka 1972 wakati huo ukitumia technolojia tofauti na ilikuwa taratibu sana tofauti nah ii ya miaka ya hivi karibuni